Ijumaa , 19th Aug , 2022

Dereva bodaboda aitwaye Hassani Abeid, ameuawa na watu wasiojulikana baada ya kumvamia na kumchoma na kitu chenye ncha kali shingoni na kumnyang’anya pikipiki yake katika mtaa wa Sawe wilayani Babati mkoani Manyara.

Bodaboda

Wakizungumza viongozi  wa bodaboda wilayani hapo wamesema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa 2:00 usiku na kusema wizi na vifo vya madereva bodaboda havitakwisha kama jeshi la polisi halitadhibiti wanaojiita deiwaka wanaojitokeza nyakati za usiku kwani ndiyo chanzo cha wizi kwa kuwa hawajasajiliwa kwenye uongozi wao na hivyo hata wakifanya tukio hawawezi kuwatambua.

Aidha wakazi wa mtaa huo wamesema kwa sasa vitendo vya mauaji katika mtaa wao vimekithiri jambo ambalo sio la kawaida.