Jumatatu , 28th Sep , 2020

Mamlaka ya kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA) imemkamata Maria Edson Mtambo (25) Mnyiha na mkazi wa Tegeta kwa Ndevu akiwa anasafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin zenye uzito wa gramu 448.12.

Mtuhumiwa huyo alikuwa akisafirisha dawa hizo kuelekea nchini India,ambapo alizihifadhi katika kifurushi cha vitabu viwili ambavyo ndani yake aliweka unga wa dawa hizo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa  hii leo Septemba 28,2020 na Kamishina Jenerali wa Mamlaka hiyo James Kaji amesema kuwa binti huyo ni mfanyakazi wa ndani huko Tegeta, na aliyekuwa anamtumia dawa hizo ni mpenzi wake raia wa nje.

Aidha Kaji amewataka vijana kuwa makini na raia wa nchi za Magharibi kwa usalama zaidi.