Jumanne , 25th Jan , 2022

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe, amemfuta kazi mkandarasi wa kampuni ya MV Consult kwa kushindwa kukamilisha ujenzi wa ghala la kisasa la kuhifadhia na kukaushia mazao ya nafaka kwa ajili ya udhibiti wa sumukuvu linalojengwa katika kijiji cha Engusero wilayani Kiteto.

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe

Akiwa ziarani katika wilaya ya Kiteto, Waziri Bashe ameonesha kutoridhishwa na kasi ya mkandarasi huyo anayejenga ghala hilo huku baadhi ya viongozi wakisema hawaoni mafanikio yoyote ya kukamilika kwa mradi huo kwa jili ya kuwanufaisha wananchi kama ilivyokusudiwa.

Mradi huo wa maghala kwa ajili ya udhibiti wa sumukuvu unajengwa katika wilaya 14 hapa nchini ambao una lengo la kuhakikisha wananchi wanaepukana na janga la sumukuvu linalosababsihwa na kuweka mahindi chini baada ya kuvuna kutokana na kutokuwa na sehemu sahihi jambo ambalo limekuwa likipelekea hasara kubwa.