Alhamisi , 16th Jun , 2016

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema kuwa asilimia 48 ya watoto wanaolawitia na kubakwa inatokea katika familia na hivyo serikali itawachukulia hatua watu wote ambao watakamatwa kwa makosa hayo.

Hayo yamesemwa leo Bungeni Mjini Dodoma na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambapo amesema serikali ya awamu ya tano imejizatiti kwa kiasi kikubwa kwaajili ya kuwalinda watoto ambapo kila atakayetiwa hatiani kwa makosa hayo atafungwa miaka 30 jela.

Aidha Waziri Mwalimu ameeleza kuwa ni vyema jamii ikatoa ushirikiano kwa vyombo husika pale wanapobaini kutokea kwa matukio hayo katika jamii.

“Nahamasisha wazazi na walezi kuongeza jitihada za kuwalinda watoto wetu kwakuwa asilimia 48 ya ubakaji na ulawiti unatoka katika majumba yetu”alisema Mwalimu

Hata hivyo amesisitiza kuwa kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya mototo wa Afrika kuwa ni ubakaji na ulawiti kwa watoto vinaepukiaka chukua hatua kuwalinda watoto.