Mkuu wa mkoa wa Mara Ally Hapi
Ally Hapi ameeleza hayo leo Jumapili Februari 6, 2022 wakati akieleza utendaji mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye yupo ziarani mkoani humo.
“Tuna wakuu wa wilaya wapya na wakurugenzi wapya lakini tunawakuu wa idara ambao bado bado wapo kwenye mfumo uleule wa upigaji waliokuwa wanawakandamiza wananchi na wanahujumu miradi ya maendeleo,” amesema Ally Hapi.
Aidha ameongeza kuwa, “Mkurugenzi wa Bunda kuna wakati anajifungia chumbani analia machozi, kila ukimuelekeza fanya hivi anakutana na wale wakuu wa idara wanampotosha,”.



