Jumapili , 13th Feb , 2022

Polisi mkoani Njombe wamemkamata Ndugu Daniel Mwilango ambaye ni mtuhumiwa wa mauaji ya Nickson Myamba (48) aliyekuwa katibu wa baraza la walei kanisa la Roman Katoliki kigango cha Parokia ya Makambako.

Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa

Mwilango amekamatwa eneo la Doma wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro.

Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa, amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa akiwa na vitu mbalimbali vya marehemeu ikiwemo simu ya mkononi.

Imeelezwa mauaji hayo yaliyotokea tarehe 8 Februari, 2022. 

Tazama Video hapo chini