Jumatatu , 1st Sep , 2014

Rais Mstaafu wa awamu ya pili nchini Tanzania, Alhaj Ali Hassan Mwinyi amezitaka nchini za Afrika Mashariki kuungana katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa saratani.

Rais Mstaafu wa awamu ya pili nchini Tanzania, Alhaj Ali Hassan Mwinyi.

Rais Mwinyi amesema hayo mjini Kampala nchini Uganda alipowasili kwa ajili ya kuongoza matembezi ya hisani kuchangia ujenzi wa wodi ya saratai katika hospital ya Mtakatifu Francis, Nsambaya Nchini humo.

Matembezi hayo yameandaliwa na taasisi ya Rotary Club na yanalenga kupunguza ukubwa wa tatizo la ugonju wa wa saratani kwa kujenga vituo vya uchunguzi na tiba.

Mwinyi ameongeza kuwa miongoni mwa magonjwa hatari yanayotishia maendeleo ya ustawi wa Afrika mashariki ni pamoja na saratani ambayo imekua ikiongezeka kwa kasi katika eneo hili