ACP Shana afariki dunia, Muhimbili waelezea

Jumatano , 16th Sep , 2020

Aliyewahi kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP Jonathan  Shana, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Septemba 16, 2020, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, alikokuwa akipatiwa matibabu.

Aliyewahi kuwa RPC Arusha, ACP Jonathan Shana

Akizungumza na EATV&EA Radio Digital mapema leo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano hospitalini hapo Aminiel Aligaesha amethibitisha hilo na kusema kuwa marehemu alikaa hospitalini hapo kwa siku 21 na kati ya hizo alikaa katika chumba cha uangalizi maalum (ICU), kwa siku tatu.

"Jonathan Shana, Mstaafu RPC Mkoa wa Arusha amefariki usiku wa kuamkia leo Septemba 16, 2020, amelazwa hapa Muhimbili kwa siku 21, na kati ya siku hizo ICU amekaa siku 3", amesema Aligaesha.

Ikumbukwe kuwa Juni 24 mwaka huu, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, alimhamisha ACP Shana kutoka kuwa RPC na kwenda kuwa afisa mnadhimu shule ya Polisi Moshi.