Waziri Ummy atoa hamasa kwa wanawake wajasiriamali

Alhamisi , 27th Aug , 2020

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu amewataka wakurugenzi wa Halmashauri kutoa mikopo mikubwa kwa wanawake wajasiriamali ili kuweza kutimiza ndoto zao hasa katika shughuli za uzalishaji Mali.

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu

Amesema kuwa hivi Sasa wanawake wamejitokeza kwa wingi akieleza kuwasilisha wazo kwa Waziri wa Fedha na mipango kuondoa  ama kushusha riba katika Taasisi za Fedha ili kuwainua wajasiriamali katika  Shughuli zao kibiashara.

Waziri Ummy ameyasema hayo leo August 27  katika mkutano uliowakutanisha wanawake wa Jumuiya ya Africa mashariki kwa kushirikiana Wizara ya Afya  na Jukwaa la wafanyabiashara wanawake (TWCC) ambapo amezindua Jukwaa la wanawake milioni 50 wafanyabishara wa kiafrica.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Hicho Jacqueline Maleko ameiomba serikali kuweka Sera ambazo zitasaidia kuwawezesha wanawake kujikwamua kiuchumi ikwemo kuweka  mikopo yenye riba nafuu ili waweze kukuza mitaji yao.

Zaidi ya nchi 38 za Africa Kati ya 54 zimetajwa kuingia katika Umoja huu Ambapo wafanyabiashara wanawake wameaswa kulitumia soko Hilo la mtandao wa wanawake barani Africa uliozinduliwa hii leo.