Jumatatu , 21st Sep , 2020

Kampuni ya mawasiliano ya simu za mikononi inayoongoza Tanzania, Vodacom Tanzania PLC imetangaza pendekezo la kutoa gawio la maalumu la shilingi 178.57 kwa wanahisa wake ikiwa ni baada ya muda mrefu kutoa gawio hilo.

 

Akizungumzia kutolewa kwa gawio hilo Afisa mtendaji wa DSE Moremi Marwa amesema kuwa huo ni muendelezo wa makampuni yaliyowekeza ikiwa na lengo la kuwapa motisha wawekezaji wake na kuwa hiyo imetolewa baada ya makubaliano na hivyo kuletaq athari chanya katika bei za hisa zake katika soko.

"Kampuni hiyo ikiwa ni miongoni mwa kampuni nyingi zilizoorodheshwa katika soko wanalazimika kufanya hivyo kwa wateja wake mara moja au mara mbili kwa mwaka kulingana na mafanikio yao katika biashara pendekezo lao litajadiliwa mwezi Oktoba kisha kutoa gawio kwa wanahisa wake" alisema

Amesema licha ya kuwepo kwa idadi ndogo ya wawekezaji wa nje katika wiki iliyoishia Septemba 18 uwekezaji uliongezeka hadi kufikia bilioni 45 ikilinganishwa na bilioni 13.3 katika wiki iliyoishia Septemba 11.