Jumatano , 4th Mei , 2022

Baadhi ya wafanyabiashara mafundi wa bidhaa za asili za samani eneo la Mwenge Dar es Salaam wamesema ni vyema sasa taasisi husika ikiwemo maliasili wakaboresha soko la ndani Kwa bidhaa za viti meza ambazo huzalisha kupitia malighafi za ndani hususani katika kipindi hiki ambacho serikali in

Ukizunguka katika maeneo mengi ya hotel migahawa viti na meza hizi za asili  Jijini hapa imekuwa maarufu sana jambo ambalo limewapa nguvu vijana hawa kufanya uwekezaji wa utengenezaji bidhaa hizi za samani licha ya changamoto ya ushindani wa soko na bidhaa kutoka nje.

"Kusema ukweli Kuna baadhi ya vitu tunavitumia hapa vingi hutoka nje ya Dar es Salaam vingine huusisha misitu hivyo zipo changamoto ya kuvipata alisema  "Eliya Nicholas - fundi/mfanyabiashara.

Amesema bidhaa wanazozalisha hutumika popote nyumbani na hata kwenye sehemu za biashara hivyo kuiomba serikali ikiwemo watu wa maliasili kuona namna ya kuwasaidia kwa urahisi upatikanaji wa malighafi ikiwemo za misitu ambazo ndiyo malighafi kubwa.

"Biashara ni ngumu na tunategemea milunda kutoka porini hivyo katika kipindi hiki Cha mvua malighafi zinkuwa shida kuzipata zinachelewa kutokana na Mvua lakini kingine watu wathamini bidhaa za ndani"Abdalah Ali-fundi fanicha