Wafanyabiashara walia na tenda za matunda

Jumanne , 1st Sep , 2020

Mara baada ya Janga la Covid 19 kuyumbisha biashara nyingi zikiwemo Hotel hii leo wafanyabiashara wa matunda katika soko la Buguruni jijini Dar es salaam wamewataka wenye hotel kuchukua tenda za matunda katika soko hilo kwaajili ya chakula na utengenezaji wa sharobati.

Eatv imefika sokoni hapo na kushuhudia Aina mbalimbali za matunda yakiwa yamejaaa sokoni hapo huku Katibu wa soko hilo bw Furahisha Kambi akishukuru wafanyabiashara na serikali kwa namna walivyoshikana kuvuka katika kipindi Cha Covid 19.

"Corona ilikuwa ni tishio kwetu na imeleta athari kubwa sana katika biashara, ila tunashukuru kwa msimamo wa serikali katika kuhakikisha kuwa mikakati ya kudhibiti inawekwa katika maeneo yote"

Aidha wafanyabiashara hao wamesema licha ya upatikanaji wa bidhaa hiyo wameiomba pia serikali Kufanya upanuzi wa soko pamoja na urekebishwaji wa mitaro ya maji katika soko hilo ili wafanyabiashara waweze kufanya biashara kwa uwazi zaidi.