Jumatano , 4th Mei , 2022

Baadhi ya wafanyabiashara na wasafirishaji jijini Dar es Salaam wamesema Kuna ulazima sasa wa serikali kuja na mpango wa makusudi wa kunusuru Hali ya maisha inayozidi kuwa ngumu Kila kukicha kutokana na kupanda Kwa Nishati ya mafuta

Rai hiyo imetolewa mara baada ya mamlaka ya udhibiti wa Nishati na Maji EWURA kutangaza bei mpya Kwa nishati ya mafuta ambayo inaanza kutumika leo mei 4,2022 bei ambayo imetajwa kutokuwa rafiki ukilinganisha na maisha halisi yalivyo

"Sisi tuko hapa tunasafirisha abiria sehemu ya buku kumpeleka mtu ukimwambia elfu mia tano ni ugomvi hivyo Biashara inazidi kuwa ngumu sana ya usafirishaji" alisema Ramadhani Juma-Mfanyabiashara/Dereva.

Wamesema kwa bei mpya ya Shilingi elfu tatu na zaidi ni maumivu makali hususani Kwa wafanyabiashara wadogo ambao hulazimika kutoa bidhaa sehemu Moja kwenda ingine huku wakiomba sasa serikali nkuingilia kati suala hili.

"Kiukweli saizi ndo tunaona maajabu   huu upandaji bei sio mchezo kama serikali haitaingilia kati hali inakwenda kuwa ngumu Sana" alisema hamisi - Mmiliki wa vyombo vya usafiri.

Kupanda kwa bei ya Nishati ya mafuta ambayo imeanza kutumika leo hadi sasa bado imekuwa na sintofahamu kutokana na gharama kuzidi kupaa juu ambapo kwa Lita Moja ya Petroli ikiuzwa shilingi 3148, dizeli 3258 na mafuta ya taa lita Shilingi 3112 Kwa Dar es Salaam hali inayofanya  Huduma zingine pia kupaa juu Zaidi