Ukweli kuhusu biashara ya vifaa ya ujenzi Tandale

Ijumaa , 4th Sep , 2020

Wafanyabiashara wa vifaa vya ujenzi na samani zilizokwisha tumika Jijini Dar es Salaam haswa katika eneo la Tandale jijini humo wamesema awali biashara hiyo ilionekana kama ya kihalifu lakini kwa sasa wanaishukuru serikali kwani usumbufu huo haupo tena kwao.

Eatv  leo imepita katika mitaa ya Tandale jijini Dar es Salaam na kushuhudia vifaa vingi vya ujenzi vilivyotumika ambapo akizungumza mfanyabiashara Ally Mkule ambaye ni mfanyabiashara wa muda mrefu sokoni hapo amesema kwa sasa ile adha ya kusumbuliwa na askari viongozi wa Halimashauri haipo tena jambo linalowafanya kuendesha  biashara hiyo kwa amani huku wakitengeneza faida kupitia biashara hiyo

Kwa upande wake Abdala Pazi amesema kuwa biashara hiyo kwa sasa imeshamiri katika maeneo mengi ya jiji amabzo zinahuisisha ununuzi wa bidhaa zilizokwishatumika na kusifu kutoa fursa za ajira kwa vijana wengi ambao wamejitenga na makundi ya uhalifu.

Aidha wafanyabiashara hao wa samani na vifaa vilivyotumika wamewataka wananchi kutokuwa na hofu kununua ama kuuza vifaa vilivyotumika kwani  serikali imewapa nafasi pekee ya mauzo ya bidhaa hizo kulingana na ubora wake.