Ukuaji wa sekta ya gesi asilia umeleta haya

Ijumaa , 2nd Oct , 2020

Ukuaji wa Sekta ya Gesi asilia na usambazaji maeneo ya mjini umeleta changamoto hasa ya usalama wa miundombinu ya gesi asilia na ile inayotumiwa na taasisi zingine katika kufanikisha huduma mbalimbali kwa wateja ambao wapo kwenye mikuza mbalimbali nchini hususani Jijini Dar es Salaam.

Picha ya Bomba la gesi

Akizungumza katika warsha ya utiaji saini mkataba wa maridhiano ya usimamizi wa pamoja wa miundombinu iliyoko chini ya ardhi kwenye mikuza (Wayleave), Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Zena amesema kuwa ni jukumu la serikali kutunga sera na kutoa miongozo inayofaa katika kusimamia rasilimali ya gesi asilia.

"Ni kazi ya Wizara ya Nishati katika sekta ndogo ya gesi asilia ni pamoja na kutunga sera na kutoa miongozo inayofaa katika kusimamia rasilimali ya gesi asilia", amesema Zena 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Mhandisi Godfrey Chibulunje, amesema kuwa maridhiano hayo yatasaidia kuja na mbinu bora za kulinda usalama wa wananchi walio jirani na mikuza.