Jumatatu , 9th Mei , 2022

Chama cha mawakili Tanzania (TLS) kimewataka  mawakili na wadau katika masuala ya Biashara kumaliza migogoro yao ya kibiashara kupitia kituo maalumu cha kimataifa cha Tanzania international Abritration center - (TIAC)

Rais wa TLS Dk. Edward Hosea

Rai hiyo imetolewa na Rais wa TLS Dk. Edward Hosea katika taarifa yake  ambapo amesema lengo la kituo hicho ni kuwasaidia wafanyabiashara kwenye utatuzi wa migogoro.

Amesema kwa kipindi cha mwaka mmoja wa Rais Samia serikali imeonyesha dira na nia ya kufungua milango ya Uwekezaji hivyo  kituo hicho kikiimarishwa kitakuwa chachu katika kuwasaidia wawekezaji.

Aidha amewataka watunga sheria kuzingatia matakwa ya sera ya nchi kibiashara ili kuondoa mgongano uliopo kati ya sheria na sera nyingi zilizopo.