Alhamisi , 31st Dec , 2020

Kampuni ya mtandao wa simu ya Tigo imetangaza washindi wawili wa millioni kumi za mchezo wa Patapata.

Kampeni ya Patapata inayoendeshwa na kampuni ya Tigo

Akizungumza na waandishi wa habari leo usiku, Meneja Uendeshaji wa The Network, Lumuliko Mengele amewataja washindi wawili wa mchezo huo kuwa  ni Mathias Januari mkazi wa Dodoma na Urembo Yusuph mkazi wa Dar es salaam.

Washindi hao wawili wa mchezo wa patapata  wamefanikiwa kujishindia shillingi million tano kila mmoja.

Aidha Meneja Biashara wa Tigopesa, Ibrahim Mfala amewahamasisha wateja na watumiaji wa mtandao wa Tigo kuendelea kucheza mchezo hyo ili waweze kushinda.