TIGO yashirikiana na Itel kuzindua Itel T20

Jumatano , 21st Oct , 2020

Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo ikishirikiana na kampuni ya Itel imezindua simu mpya ya Itel T20 itakayowarahisishia wateja wao katika matumizi ya  mtandaoni (Internet).

Kushoto ni Meneja wa bidhaa za internet wa Tigo, Mkumbo Myonga, na kulia ni Afisa Habari wa Kampuni ya simu ya Itel Fernando Wolle wakionyesha simu mpya waliyoizindua leo Itel T20

Akizungumza na wandishi wa habari leo Meneja wa bidhaa za internet wa Tigo, Mkumbo Myonga, amesema kuwa bidhaa hiyo yenye ubora wa aina yake itakua ni chaguo sahihi kwa wateja wa mtandao wa tigo kutokana na urahisi wake katika matumizi ya Mtandao imetokana na ushirikiano wake na  kampuni ya simu ya Itel.

"Tigo kwa kushirikiana na Kampuni ya simu ya Itel tumewaita hapa kwa ajili ya kuzindua simu mpya aina ya smartphone ambayo inaitwa Itel T20 ushirikiano huu unakuja ikiwa ni muendelezo wa kuwaletea wateja wetu bidhaa mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya internet, huu ni ushirikiano unatuleta kwenye nafasi nzuri ya kuweza kuwahudumia wateja wetu” amesema Mkumbo Myonga

Kwa upande wa Afisa Habari wa Kampuni ya simu ya Itel Fernando Wolle alikuwa na haya yakusema kuhusiana na ushirikiano huo pamoja na jina la simu hiyo, "Tumeungana leo na Tigo illikuwawezesha wateja waweze kufurahia maisha ya kidigitali, unaweza jiuliza kwanini simu inaitwa Itel T20, tumechukua T ikimaanisha Tigo na 20 ni mwaka 2020 kwahiyo Itel T20 ni Itel Tigo 2020” amesema Fernando Wolle