Jumatatu , 20th Sep , 2021

Wananchi wa Bangkok, Thailand wameamua kutengeneza bustani ya maua na mboga  kwenye teksi zilizoachwa na madereva  baada ya Taifa hilo kuweka vizuizi kutokana na mlipuko wa COVID-19 na kulazimika kuyaegesha.

Picha ya Teksi iliyopandwa Maua

Wameanzisha mradi huo wa maua na mboga mboga kama sehemu ya kukuza vipato vyao na madereva ambao hawana kazi hivi sasa kwani biashara ya teksi mjini hapo hutegemea watalii kwa sehemu kubwa.