Jumapili , 14th Mar , 2021

Kampuni ya Kubashiri ya Meridian Bet imetoa msaada wa vifaa tiba kwa Wanaougua uti wa mgongo nchini kutokana na kuwepo kwa changomoto ya wagonjwa wa uti wa mgongo  wengi ya kutomudu gharama ya vifaa tiba.

Afisa Huduma wa jamii wa Meridian Bet,  Amani Maeda na Meneja mwendeshaji, Corrie Borman wamekabidhi msaada wa vifaa tiba mbalimbali kwenye Taasisi ya watu wanaougua uti wa mgongo nchini.

Akizungumza, Maeda amesema kampuni yao imeendelea kutoa mkono wa faraja kwa wahitaji na jana imekabidhi vifaa tiba ikiwamo Urine bags, malt external catheter na sanitary pads kwenye Taasisi hiyo nchini.

Akizungumza kwa niaba ya mwenyekiti wa Taasisi , Haidan Shayo, mmoja wa wanachama, Abdul Ally alisema wagonjwa wengi wa uti wa mgongo wamekuwa na changamoto ya kumudu gharama ya vifaa tiba.

"Wenye changamoto hii uwa tunashindwa ku-control haja, hivyo tunahitaji kuwa na 'urine bag' au pempars ili kujistri, lakini kutokana na gharama kuwa kubwa, wengi wetu tunalazimika kutumia khanga," alisema Ally jana wakati akipokea msaada wa Meridian Bet.

Mwanachama mwingine, Masha Mbise ambaye aliugua uti wa mgongo baada ya kugongwa na gari aliishukuru Meridian Bet kwa sapoti hiyo na kuziomba kampuni nyingine kuiga mfano wa Meridian Bet.