Jumatatu , 25th Oct , 2021

Serikali ya Luxemburg huko barani ulaya imepitisha sheria mpya ambayo itaruhusu uuzaji na ununuaji wa mbegu za bangi madukani.

Picha ya mmea wa Bangi

Kupitia sheria hiyo iliyowasilishwa na baraza la mawaziri, wakazi wenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea wataruhusiwa kisheria kupanda hadi mimea minne ya bangi katika bustani zao kwa kila kaya kwa matumizi binafsi.

Chini ya sheria hiyo mpya itaifanya Luxemburg kuwa nchi ya kwanza katika jumuiya ya nchi za umoja wa ulaya kuhalalisha utengenezaji na utumiaji wa bangi, ambapo itaungana na nchi zingine ulimwenguni kama vile Uruguay na Canada katika uhalalishaji wa bangi