Moja ya changamoto inayowakwamisha wafanyabiashara wa mboga mboga ni pamoja na kukosa soko la uhakika huku kwa wakulima nao wakikumbana na kikwazo cha ukosefu wa maji ya uhakika kumwagilia mazao yao.
Huyu ni miongoni mwa vijana wachache walioamua kuachana shughuli za kuuza mitumba na kuamua kufanya biashara ya kuuza mboga mboga na kuziandaa shambani akielezea jinsi biashara hii ilivyomnufaisha.
Syrus amesema ni vyema serikali ikatoa maeneo ambayo vijana wenye nia ya kujiajiri katika shughuli za uzalishaji mali kwa kuwa yapo mabonde mengi ambayo yakiandaliwa vizuri yanaweza kuajiri vijana wengi zaidi.
Sina amewaomba wadau wenye uwezo wa kuchimba visima vya uhakika wa kupatikana maji mwaka mzima kujitokeza ili kuwezesha kupatikana kwa maji ya umwagiliaji kwa muda wote.