Jumatatu , 20th Sep , 2021

Toleo jipya la iPhone 13 Pro na 13 Pro Max ambazo zimetolewa wiki iliyopita, zimeboreshwa zaidi hasa kwenye ubora wa kurekodi video na picha, kioo ambacho ni ‘Super Retina XDR’ na ‘ProMotion’ ambapo kasi yake mwaka huu imebadilika kutoka 10Hz hadi 120Hz. 

Picha ya Simu aina ya iPhone

Mabadiliko hayo ya Teknolojia yanatoa uwezo mpya wa kuvutia wa simu hizo, huku pia zikiwa zimeongezewa mfumo wa 5G, chaji kukaa muda mrefu na uwezo mpya wa kuhifadhi hadi kufikia 1TB.