Alhamisi , 21st Oct , 2021

Mtandao wa Instagram umefanya maboresho mapya ambapo watumiaji watakuwa na uwezo wa ku-post, ku-upload video na picha katika akaunti zao za Instagram kwa kupitia tovuti/website ya Instagram. 

Picha ikionyesha maboresho ya ku-post Instagram kwa kutumia website

Maboresho haya yatakuwa msaada mkubwa kwa watu wengi sana hasa kwa wanaosimamia akaunti za watu ambao wanatumia kompyuta katika shughuli mbalimbali na kupunguza matumizi ya simu, featurehii imeanza kutumika wiki hii kwa baadhi ya watumiaji na itaendelea kutoka taratibu kwa watumiaji wengine.