Jumatano , 13th Oct , 2021

Kufuatia tatizo la kimtandao ambalo lilitokea siku za hivi karibuni na kuzua taharuki kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii, sasa Instagram imeanza majaribio ya programu 'feature' mpya ambayo itakuwa ikitoa taarifa pale linapojitokeza tatizo la kiufundi.

Picha ya 'feature' inayofanyiwa majaribio na Instagram

Taarifa hiyo itakuwa ikitokea kwa mfumo wa notification kwenye ukurasa wa mtumiaji wa mtandao huo kumjulisha kuwa limejitokeza tatizo la kiufundi ambapo baada ya mafanikio huduma hiyo itasambaa ulimwenguni kote.