Jumatatu , 9th Mei , 2022

Taarifa kutoka soko la hisa la Dar es salaam imeonyesha kushuka bei hisa zake sokoni kutokana na myumbo uliopo kwenye kupanda kwa bei za bidhaa hali inayosababisha wawekezaji kuchukua tahadhari katika kufanya uwekezaji.

Mtendaji Mkuu wa soko la hisa Moremi Marwa

Mtendaji Mkuu wa soko hilo Moremi Marwa amesema kwa wiki hii kumekuwepo na  punguzo la ukuaji wa mtaji sokoni la bilioni 12 kutoka trillion 10.2 tarehe 29 April hadi kufikia trillion 10.19 mnamo tarehe 6 Mei 2022..

Aidha Katika upande wa Hatifungani zilizoorodheshwa sokoni zimebakia katika kiwango cha trillion 15.71 huku hati fungani za muda mrefu hususani za miaka kumi na mitano za serikali zikiendelea kuaminiwa zaidi na wawekezaji.

Kuhusu mchanganuo wa uwekezaji asilimia 25 ya Uwekezaji kwa upande wa manunuzi ulichangiwa na wawekezaji wa ndani wa nje wakichangia asilimia 75 katika upande huo,ambapo 28 asilimia ya Mauzo ikichangwa na wawekezaji wa ndani na asilimia 72 kutoka nje hivyo kufanya soko kutawaliwa na wawekezaji kutoka nje kwenye Mauzo na manunuzi.