Jumatano , 20th Oct , 2021

Kampuni kubwa ya mtandao wa kijamii wa Facebook inapanga kubadilisha jina la kampuni yake kuanzia wiki ijayo ili kuonesha mabadiliko yake kwa lengo la kujenga kile kinachoitwa “Metaverse”.

Picha ya Mark Zuckerberg Mkurugenzi Mtendaji wa Facebook

Afisa mkuu mtendaji wa Facebook, Mark Zuckerberg ana mpango wa kuzungumzia juu ya mabadiliko ya jina na kuweka wazi jina jipya kwenye mkutano wa kila mwaka wa kampuni hiyo wa “Annual Connect Conference” tarehe 28 Oktoba mwaka huu.