EATV yaendelea kukabidhi makapu wiki ya wateja

Jumatano , 7th Oct , 2020

Kituo cha redio cha East Africa Radio, kupitia kipindi chake cha Supa Breakfast, kwa Kituo cha redio cha East Africa Radio, kupitia kipindi chake cha Supa Breakfast, kwa kushirikiana na Royal Oven Bakery, kimekabidhi zawadi kwa mtoa huduma bora wa pili-

Muandaaji wa kipindi cha SupaBreakfast cha East Africa Radio, Mackriner Siyovelwa akimkabidhi zawadi kutoka Royal Oven Bakery mfanyakazi wa S. H. AMON Faraja Ezekiel.

kutoka duka kubwa la vipodozi la S.H. AMON tawi la Mlimani City baada ya  kuibuka mshindi kwa kutoa huduma bora kwa wateja.

Kampeni hiyo ya kuwazawadia watoa huduma bora katika Wiki ya Huduma kwa Wateja inaendeshwa kupitia wasikilizaji wa East Africa Radio, ambao hupiga simu na kuelezea namna ambavyo walipatiwa huduma bora na mtu aliyewahudumia katika taasisi husika na walivyosaidiwa kutatua tatizo lao.

Akizungumza baada ya kupatiwa kapu hilo liloloshehena aina mbalimbali ya vitafunwa vya kifungua kinywa, Faraja Ezekiel kutoka S. H. AMON, amesema kuwa mteja kwao ni mfalme na wamekuwa wakitoa huduma kwa kusikiliza mteja anataka nini kwa wakati huo.

Kwa upande wake Msimamizi wa S.H. AMON, Salama Nasoro amesema kuwa anaona faraja kwa mfanyakazi mwenzake kuchaguliwa na mteja ambaye huenda hata wao hawamkumbuki ila huduma yao imecha alama kwake, hivyo kuwasihi wafanyakazi wote kutoa huduma kwa upendo kwa wateja katika biashara yoyote.