"Rushwa sio maadili ya Jeshi la Polisi" - ACP
Askari wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Songwe, wametakiwa kuendelea kutoa huduma bora kwa jamii ikiwa ni pamoja na kuzingatia maadili ya kazi pindi wanapotekeleza majukumu yao ya kusimamia sheria za usalama barabarani kwa lengo kuendelea kujenga taswira nzuri ya Jeshi la Polisi.