Askofu Pengo awataka watanzania kuitunza amani
Askofu mkuu wa kanisa katoliki jimbo kuu la Dar es salaam Kardinali Polycarp Pengo amewataka watanzania kuhakikisha siasa na harakati za uchaguzi haziwatengi na kuwagawanya kimakundi na kuondoa amani baada uchaguzi.