Upasuaji washindikana kwa kukosa umeme Uyui Tabora
Jengo la upasuaji lililojengwa kwenye Kituo cha Afya kilichopo Kata ya Upuge, Wilayani Uyui mkoani Tabora, linashindwa kutoa huduma zake kwa ufasaha kutokana na kata hiyo kutokuwa na huduma ya umeme wa shirika la umeme nchini Tanzania (Tanesco).