Wanasiasa watakiwa kuacha tofauti katika maendeleo
Viongozi wa madhehebu mbalimbali yaliyopo wilayani Meatu mkoani Simiyu wamewaomba wanasiasa ambao hawakubahatika kushinda katika nafasi za udiwani na ubunge kuondoa tofauti zao na badala yake waungane katika kuwaletea maendeleo wananchi.