Wakazi wa Mtwara waingiwa hofu kuhusu mita 200
Kufuatia kutoelewana kuhusu suala la kusimama umbali wa mita 200 kutoka eneo la kupigia kura, baadhi ya wananchi wa manispaa ya Mtwara Mikindani wameanza kushikwa na hofu juu ya usalama wao kiasi cha kulazimika kukimbia mji.