Mashindano ya tenisi ya vijana kufanyika Novemba
Chama cha Tenisi Tanzania TTA kimeandaa mashindano ya wazi ya mchezo huo kwa vijana walio chini ya miaka 18 yanayotarajiwa kuanza Novemba mwaka huu jijini Dar es salaam kwa kushirikisha timu za wanawake na wanaume.