Mafuriko yaua wawili Mwanza, Airport yafungwa
Watu wawili wamefariki dunia kutokana na kukumbwa na mafuriko ya mvua kubwa iliyonyesha kwa masaa kadhaa jijini Mwanza, akiwamo mwanafunzi wa kidato cha nne aliyesombwa na maji wakati akiwahi kufanya mitihani ya mwisho.