Mkapa; Wazazi wahimizeni watoto kupenda elimu
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu nchini Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa, amewataka wazazi wa mikoa ya Kusini mwa Tanzania kutoa msukumo kwa watoto wao kujali umuhimu wa elimu, ili wanufaike na uwekezaji unaoendelea katika mikoa hiyo.