Simba kujadili mgogoro wa makocha, Matola ajiuzulu
Kamati ya utendaji ya Klabu ya Simba SC inatarajia kukutana siku yoyote kuanzia sasa kuweza kujadili mgogoro uliopo kati ya kocha mkuu wa klabu hiyo Dylan Kerr na msaidizi wake Suleiman Matola uliopelekea Matola kujiuzulu kuifundisha klabu hiyo.