Mkwasa atoa changamoto kwa klabu nchini
kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania Charles Boniface Mkwasa amezitaka klabu za soka hapa nchini kuruhusu wachezaji wao kwenda nje ya nchi kucheza soka la kulipwa endapo nafasi zitatokea ili kuwapa uzoefu wa mechi za kimataifa.