Serikali yasema Kipindupindu bado tatizo nchini
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia watoto na wazee imesema kuwa bado kuna maambukizi mapya ya ugonjwa wa kipindupindu hapa nchini, na kusisitiza kuwa agizo lake la kupiga marufuku uuzwaji wa matunda pamoja na chakula lipo pale pale.

