Rais Mstaafu Ufaransa aanza kutumikia kifungo
Rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy leo ameanza kutumikia kifungo cha miaka mitano gerezani baada ya kuhukumiwa kwa uhalifu wa kula njama ya kufadhili uchaguzi wa mwaka 2007 kinyume na sheria kwa kutumia fedha zilizotoka kwa aliyekuwa kiongozi wa Libya Muamar Gaddafi.

