Ukubwa wa mtaji katika soko la hisa waongezeka
Ukubwa wa mtaji katika Soko la Hisa la Dar es Salaam DSE umeongezeka kwa asilimia mbili kutoka fedha za Tanzania shilingi trilioni 23.5 hadi shilingi trilioni 24 kwa mujibu wa taarifa ya mauzo katika soko hilo kwa kipindi cha juma moja lililopita.
