Prof. Mbarawa aingilia kati mgogoro wa KIA
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amewataka wananchi wanaozunguka eneo la uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), kuwa watulivu katika kipindi hiki ambacho Serikali inatafuta ufumbuzi wa kudumu wa mgogoro.