Serikali, wadau kujadili sheria mpya ya habari
Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imepanga kukutana na wadau wa habari nchini ili kujadili mapungufu yaliyopo kwenye sheria ya huduma ya habari nchini lengo likiwa ni kuongeza ufanisi katika utendaji wa vyombo vya habari.