Makontena mengine ya mchanga wa dhahabu yanaswa

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko, akiongela kubainika kwa makontena yenye mchanga wa dhahabu 262 katika bandari ya Dar es salaam leo tarehe 25 Machi, 2017 Wengine katika picha ni maafisa wa TPA na Kamanda wa Polisi Kikosi cha Bandari Ramadhani Mungi
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imebaini makontena mengine 262 yenye mchanga wa dhahabu yaliyokuwa yamehifadhiwa katika bandari kavu ya MOFED (zamani ZAMCARGO) iliyopo Kurasini jijini Dar es salaam.
