Mahakama yatoa maamuzi juu ya Nabii Tito
Mahakama ya Wilaya ya Dodoma imemuamuru Mkuu wa Gereza la Isanga kumpeleka hospitali kuu ya magonjwa ya akili (Mirembe), mkazi wa kijiji cha Nong'ona Tito Onesmo Machibya maarufu kama (Nabii Tito), ili kuchunguzwa kama ana ugonjwa wa akili au la.

