Portland yaongoza mbio za robo fainali
Timu ya Kikapu ya Portland kutoka Kinondoni imeongoza mbio za kuelekea robo fainali ya Sprite Bball Kings 2018 baada ya kushinda kwa vikapu 126 dhidi ya 54 vya Mbezi Beach KKKT kwenye mchezo uliopigwa kwenye viwanja vya Airwing Ukonga jioni ya leo.