Serikali kuwapima vilevi wafanyakazi
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe, amesema serikali haitaendelea kuvumilia kuona watu wanakufa kutokana na ajali zinazotokana na makosa ya kibinadamu ikiwemo ulevi na imekuja na mpango wa kuwapima vilevi madereva.