Mahiga atoa ufafanuzi sakata la wizi ofisi ya DPP
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt Augustine Mahiga, amesema kuwa kompyuta zilizopo kwenye ofisi ya DPP hazijaibiwa, bali kilichoibiwa ni vipande vya Kompyuta kutoka ofisi ndogo ya mkoa na kwamba nyaraka zote za wahujumu uchumi, waliokiri na wanaoendelea kukiri makosa yao ziko salama.

