TLS kukutana na Rais kumwambia yanayoendelea
Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimetangaza kitaanzisha kamati maalum itakayoratibu mpango wa kukutana na Rais Samia Suluhu Hassan kwa lengo la kujadili na kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazohusiana na masuala ya kisheria, haki za binadamu na utawala bora.