Baraza la Mawaziri Madagascar lavunjwa
Rais wa Madagascar, Andry Rajoelina, ametangaza kulivunja baraza lake la mawaziri kufuatia maandamano mabaya Zaidi kuripotiwa kwenye kisiwa hicho, raia wakipinga kukatika kwa umeme mara kwa mara pamoja na uhaba wa maji, watu 22 wakiripotiwa kufa tangu yalipoanza wiki iliyopita.

